Tenzi za Rohoni 156 – Bwana Yesu Yuko Wapi
Tenzi Na. 156
Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 156, “Bwana Yesu Yuko Wapi”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza.
Maneno ya Wimbo
1. Bwana Yesu yuko wapi,
mpenzi wangu rafiki?
Njia gani amekwenda?
Nitamwonaje mimi?
Roho yangu yajutishwa
na dhambi na huzuni.
Yesu, mpenzi wangu mwema,
namtafuta kwa bidii.
2. Ninapaza sauti yangu,
nalia: Wapi Yesu?
Ndani mwangu sina raha
mpaka nimwone Yesu.
Ningekuwa na mabawa,
ningeruka upesi
milimani, mabondeni,
kumtafuta Bwanangu.
3. Aondoa shida zangu,
maharibifu yote.
Nikiona taabu mimi,
anituliza yeye.
Nitafanya bidii sana
kumtafuta popote;
sitachoka kutembea
mchana hata usiku.
4. Bwana Yesu nitokee,
roho inakuita.
Niondoe na maovu,
Yesu Mwokozi wangu.
Utulize hamu yangu,
kaa kwangu daima.
Nikupende sana wewe,
niwe wako milele.