Tenzi za Rohoni 158 – Aniongozapo Pote
Tenzi Na. 158
Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 158, “Aniongozapo Pote”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza.
Maneno ya Wimbo
KIITIKIO:
Nitaongozwa na Bwana
usiku kucha na mchana,
Yesu, rafiki wa heri;
ninakumbuka Kalvari.
1. Aniongozapo pote,
nimwandame siku zote.
Kwa ajili yangu mimi
aliuawa Kalvari.
2. Lanitosha Neno lake,
nishikwe na mkono wake.
Mapenzi yake ni heri,
yalitimizwa Kalvari.
3. Nitaendelea mbele
pamoja naye milele.
Pendo lake ni hiari,
Bwana Yesu wa Kalvari.