Tenzi za Rohoni 152 – Uliyesulibishwa
Tenzi Na. 152
Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 152, “Uliyesulibishwa”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza.
Maneno ya Wimbo
1. Uliyesulibishwa,
Mtakatifu Bwanangu,
uwe ngao shidani,
uniombee mimi.
Uliyesulibishwa,
Mtakatifu Bwanangu!
2. Wongofu sina hata,
niondolee makosa.
Mwovu akinishtaki,
nasumbuka rohoni.
Wongofu sina hata,
niondolee makosa.
3. Wewe tu nipokee,
nakukimbilia wee.
Hata nifanye bidii,
nikatoe machozi:
Wewe tu nipokee,
nakukimbilia wee.
4. Uwe ngao shidani,
niombee na mimi!
Hapa nikiumizwa,
saa ya mwisho ikija:
Uwe ngao shidani,
niombee na mimi!