Skip to main content

Tenzi za Rohoni 151 – Usiku Mtakatifu

Tenzi za Rohoni 151 – Usiku Mtakatifu

Tenzi Na. 151

Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 151, “Usiku Mtakatifu”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza.


Maneno ya Wimbo

1. Usiku mtakatifu!
Wengine walala,
wakeshao ni Yosefu tu
na Maria waliomlinda
Yesu, mwana mzuri,
Yesu, mwana mzuri.

2. Usiku mtakatifu!
Wachunga wapewa
habari nzuri na malaika,
zienezwe popote sasa:
Yesu Mponya kaja,
Yesu Mponya kaja.

3. Usiku mtakatifu!
Siku ya furaha
imetuangaza Kimungu.
Tumeupewa ukombozi:
Kristo amefika,
Kristo amefika.


Tazama Tenzi za Rohoni 1–164


Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

Scroll to Top