Skip to main content

Tenzi za Rohoni 148 – Ondokeni! Tunaitwa

Tenzi za Rohoni 148 – Ondokeni! Tunaitwa

Tenzi Na. 148

Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 148, “Ondokeni! Tunaitwa”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza.


Maneno ya Wimbo

1. Ondokeni! tunaitwa
na walinzi wa juu mnarani.
Yerusalemu, amka wee!
Ni usiku wa manane,
yuaja Bwana wa arusi,
wanawali wako wapi?
Amkeni upesi!
Kaziwasheni taa.
Haleluya!
Fuateni arusini
kwenda kumpokea Bwana!

2. Sayuni anasikia
moyo waruka kwa furaha,
yu macho, anaondoka.
Mponya wake anashuka
mbinguni mwenye utukufu,
aleta mwanga wa kweli;
taji yake yaja
na Mwana wa Mungu.
Hosiana!
Twafuata kwenye shangwe
tukale karamu yake.

3. Waimbiwa nyimbo nzuri
kwa misemo ya watu wote
na ya malaika mbinguni.
Tukifika mjini kwako
kwenye milango ya malulu,
tutakuimbia nasi.
Furaha kama hii
haijasikiwa
duniani.
Nasi sasa tunaimba,
tunakusifu, Ee Bwana.


Tazama Tenzi za Rohoni 1–164


Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

Scroll to Top