Tenzi za Rohoni 146 – Neno La Mungu Takata
Tenzi Na. 146
Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 146, “Neno La Mungu Takata”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza.
Maneno ya Wimbo
KIITIKIO:
/: Twakushika siku zote
maishani na kufani. :/
1. Neno la Mungu takata
lililotoka mbinguni,
ambalo moto na panga
haziwezi kulishinda.
2. Waliotutangulia,
waliokutegemea,
wamekufia mashujaa;
nasi tulio watoto,
3. Neno la Mungu takata,
tukushuhudie nasi
kwa neno tamu na tendo
kunako wenzi au adui.