Skip to main content

Tenzi za Rohoni 145 – Ndoa Yetu Nzima

Tenzi za Rohoni 145 – Ndoa Yetu Nzima

Tenzi Na. 145

Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 145, “Ndoa Yetu Nzima”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza.


Maneno ya Wimbo

KIITIKIO:
/: Ndoa yetu,
Bwana,
ndiwe baraka! :/

1. Ndoa yetu nzima
simika, Yesu!
Usiku na mchana
uwepo kwetu.
Leo tuna raha,
wewe watupa.

2. Atoka kijana,
ataka mchumba.
Siku zinapita
za kupimana.
Leo twapatana
pamoja kukaa.

3. Vyote hapa chini
vinakaa muda,
vyote vinaoza,
tena vyachakaa.
Pendo la dunia
nalo huchakaa.

4. Kaa kwetu, Bwana,
Kutukagua,
pendo letu sisi
lisichakae;
hivi na tukae
na baraka tu.

5. Kana arusini
ulialikwa.
Walivyoishiwa,
ukaongeza,
nasi shida zetu
utazishinda.


Tazama Tenzi za Rohoni 1–164


Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

Scroll to Top