Tenzi za Rohoni 133 – Ni Wako Mungu!
Tenzi Na. 133
Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 133, “Ni Wako Mungu!”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza.
Maneno ya Wimbo
Ni wako Mungu!
Ni furaha kwangu,
Ni raha kumjua mwokozi wangu.
Aleluya enzi ndako;
Aleluya,Amin.
Aleluya,enzi ndako;
Rejea Yesu.
Mwana wa Mungu
Ndiye fungu langu,
Na moyo hufurahi kwa Yesu wangu.
Raha ya kweli
Ina jina hili,
Na aliyeshika,ana Mbingu kweli.
Nimeingia
Mapendano haya,
Nimepata uzima na Mbingu pia.
Nilipo chini,
Ni mwako kazini
Hata nije kwako uliko Mbinguni.