Tenzi za Rohoni 131 – Piga Sana Vitu Vyema
Tenzi Na. 131
Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 131, “Piga Sana Vitu Vyema”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza.
Maneno ya Wimbo
Piga sana vita vyema
Kwa ushujaa daima,
Yesu ndiye nguvu zako,
Yesu ndiye kweli yako.
Kaza mwendo, ushindane
Angaza macho, umwone
Yesu ndiye njia yako,
Naye ndiye tuzo lako.
Tupa kizito, simama,
Tazama mbele, si nyuma;
Ni yeye uzima wako,
Naye ni kipendo chako.
Tangamka, uamini
Akushika mikononi
Hageuki, akupenda,
Kuwa naye una pia.