Tenzi za Rohoni 161 – Usiku Uingiapo
Tenzi Na. 161
Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 161, “Usiku Uingiapo”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza.
Maneno ya Wimbo
1. Usiku uingiapo,
umwaze Mungu Mkuu
aendeshaye dunia
kwa mwendo mtulivu.
2. Kwa nini wahangaika
usiku na mchana?
Umtwishe huzuni yako
aliyekuumba.
3. Kwake haujapunguka
uwezo na msaada.
Atatimiza yote
aliyoyaanza.
4. Ukamwachie kutenda
atakalo kwako!
Kwa hiyo ulale raha
na kufurahiwa.