Skip to main content

Tenzi za Rohoni 139 – Nuru Ya Rohoni

Tenzi za Rohoni 139 – Nuru Ya Rohoni

Tenzi Na. 139

Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 139, “Nuru Ya Rohoni”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza.


Maneno ya Wimbo

1. Nuru ya rohoni
ni Bwana Yesu.
Nakuomba sana
niangazishe;
ukanitazame
kwa huruma tu,
/: Ukanitulize
mimi maskini. :/

2. Futa dhambi zangu
kwa damu yako.
Hasira ya Mungu
iniondoke.
Machubuko yako,
hata mateso,
/: Niyawaze vema
rohoni mwangu. :/

3. Nakutumaini
peke yako tu,
niwe mtumwa wako
pote nilipo,
utanikubali,
sina mashaka!
/: Nitakushukuru
pasipo mwisho. :/


Tazama Tenzi za Rohoni 1–164


Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

Scroll to Top