Tenzi za Rohoni 137 – Yesu Mponya
Tenzi Na. 137
Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 137, “Yesu Mponya”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza.
Maneno ya Wimbo
Yesu ndiye mganga wetu
Aponya wagonjwa wote;
Mganga wetu ni Yesu,
Aponyaye hasira.
Tumsifu huyo Yesu
Tumsifu milele,
Kwani Mponya mtakata
Mwokozi wa wanyonge
Mganga wetu ni Yesu
Huondoa matusi;
Mganga wetu ni Yesu,
Mwenye kuponya choyo.
Mganga wetu ni Yesu
Huponya wivu wetu;
Yesu ndiye aponyae
Kelele za nyumbani.
Mganga wetu ni Yesu
Mponya wa tamaa mbaya;
Mganga wetu ni Yesu
Uasherati hufuta
Mganga wetu ni Yesu
Aponya kiu cha pombe,
Mganga wetu ni Yesu
Kila dhambi uponya