Skip to main content

Tenzi za Rohoni 136 – Msifuni, Yesu Ndie Mkombozi

Tenzi za Rohoni 136 – Msifuni, Yesu Ndie Mkombozi

Tenzi Na. 136

Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 136, “Msifuni, Yesu Ndie Mkombozi”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza.


Maneno ya Wimbo

Msifuni ,Yesu ndiye mkombozi;
Imbeni ya pendo zake kuu,
Sujuduni,malaika mlioko,
Jina lake liwe na sifa kuu.
Kama vile mchunga uchungavyo
Vivyo sisi kutwa atachunga.
Msifuni mlio wakw watoto
Msifuni aliye mchunga.
Msifuni,Yesu ndiye mkombozi;
Akateswa tupate ongoka;
Ndiye Mwamba,Dhamana ya kuokoka;
Sujuduni kwake muangikwa,
Yesu aliyeudhiwa na hamu
Kwa pendo za baba yake Mungu.
Aliyefyolewa na kusulubiwa.
Msifuni ndilo letu fungu.
Msifuni,Yesu ndiye Mkombozi;
Shindukeni,enyi malango juu;
Bwana Yesu tangu milele Mwokozi,
Mvikeni taji, ni yake tu.
Atakuja kuitawala nchi,
Yesu,Mwombezi wetu wa Mungu.
Msifuni, ni mfalme wa salama;
Ndiye kweli mwana wake Mungu.
Msifuni, ni mfalme wa salama;
Ndiye kweli mwana wake Mungu.


Tazama Tenzi za Rohoni 1–164


Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

banner
Scroll to Top