Skip to main content

Tenzi za Rohoni 134 – Juu Yake Langu Shaka

Tenzi za Rohoni 134 – Juu Yake Langu Shaka

Tenzi Na. 134

Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 134, “Juu Yake Langu Shaka”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza.


Maneno ya Wimbo

Juu yake langu shaka,
Yesu namuwekea,
Nami sitafedheheka
Nikimtegemea.
Natumai, natumai,
Nnatumai kwake tu;
Natumai, natumai,
Natumai kwake tu.
Juu yake, dhambi zangu;
Aniosha kwa damu;
Nionekane kwa Mungu,
Nisiye na laumu.
Juu yake yangu hofu;
Kwake nimetulia;
Sipotei kwa upofu
Njia aning’azia.
Juu yake raha yangu;
Humuangalia tu;
Mwenye kila ulimwengu,
Aniruzuku na huu.
Juu yake, moyo wangu;
Hali yangu na mali;
Mimi wake, Yeye wangu,
Twapasana kamili.


Tazama Tenzi za Rohoni 1–164


Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

banner
Scroll to Top