Skip to main content

Tenzi za Rohoni 128 – Mmoja Apite Wote

Tenzi za Rohoni 128 – Mmoja Apite Wote

Tenzi Na. 128

Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 128, “Mmoja Apite Wote”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza.


Maneno ya Wimbo

Mmoja apita wote,
Atupenda;
Zaidi ya ndugu wote,
Atupenda;
Rafiki wa duniani,
Wote hatuwaamini;
Yesu kwa kila zamani,
Atupenda.
Kumjua ni uzima,
Atupenda;
Jinsi ajaavyo wema
Atupenda;
Yeye ametununua
Kwa damu aliyomwaga,
Dhambini kutuokoa,
Atupenda.
Sasa tunaye rafiki,
Atupenda;
Hupenda kutubariki;
Atupenda;
Twapenda kumsikia,
Atwita kukaribia,
Nasi tutamwamania,
Atupenda.
Husamehe Dhambi zetu,
Atupenda;
Hushinda adui zetu,
Atupenda;
Anatwonea huruma,
Hatupati ila mema,
Anatwongoza salama,
Atupenda.


Tazama Tenzi za Rohoni 1–164


Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

Scroll to Top