Skip to main content

Tenzi za Rohoni 126 – Ni Mji Mzuri

Tenzi za Rohoni 126 – Ni Mji Mzuri

Tenzi Na. 126

Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 126, “Ni Mji Mzuri”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza.


Maneno ya Wimbo

Ni mji mzuri,
Mbali sana;
Watu wanawiri
Kama jua;
Waimba kwa tamu,
Tuna wema hakimu:
Sifa na idumu,
Kwake Bwana.
Ni mji mzuri
Twende sote!
Una na fahari
Msikawe!
Raha tutaona,
Dhambi hapana tena;
Hatutaachana
Siku zote.
Ni mji mzuri;
Macho yote
Huko wanawiri
Kama pete;
Baba tutamwona,
Tukifanywa tu wana;
Tumo kupendana
Naye sote.
Ni mji mzuri;
Tusipotee
Na tuwe hodari,
Tuupate!
Tufunze, tutume
Kwa taji na ufalme:
Sifa na zivume
Siku zote.


Tazama Tenzi za Rohoni 1–164


Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

Scroll to Top