Skip to main content

Tenzi za Rohoni 125 – Ati Twonane Mtoni?

Tenzi za Rohoni 125 – Ati Twonane Mtoni?

Tenzi Na. 125

Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 125, “Ati Twonane Mtoni?”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza.


Maneno ya Wimbo

Ati twonane mtoni?
Maji mazuri ya Mbingu;
Yanatokea mwangani,
Penye kiti cha Mungu.
Naam, twonane mtoni!
Watakatifu, kwenu ni mtoni!
Tutakutanika mtoni
Penye kiti cha Mungu.
Tukitembea mtoni
Na Yesu mchunga wetu
Daima tu ibadani
Usoni pake kwetu.
Kwang’ara sana mtoni
Cha Mwokozi ni kioo,
Milele hatuachani,
Tumsifu kwa nyimbo.
Si mbali sana mtoni,
Karibu tutawasili,
Mara huwa furahani
Na amani ya kweli.


Tazama Tenzi za Rohoni 1–164


Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

Scroll to Top