Skip to main content

Tenzi za Rohoni 123 – Nimeketi Mimi Nili Kipofu

Tenzi za Rohoni 123 – Nimeketi Mimi Nili Kipofu

Tenzi Na. 123

Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 123, “Nimeketi Mimi Nili Kipofu”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza.


Maneno ya Wimbo

Nimeketi mimi nili kipofu
Gizani nangojea macho;
Ewe Bwana Yesu mwenye wokovu,
Ondoa dhambi zangu nzito.
Huruma hakuna aonaye,
Gizani nagojea macho,
Sasa nitakase nikusihiye,
Yesu, na dhambi zangu nzito.
Tangu siku nyingi nimepofuka
Natamani uso nikwone;
Ewe Bwana Yesu, mwenye baraka
Sema neno, basi, nipone.
Nimeketi mimi nili na giza,
Nami ya kutumai sina;
Ili nasikia kunong’oneza,
“Kwake Yesu kuna kupona.”


Tazama Tenzi za Rohoni 1–164


Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

banner
Scroll to Top