Skip to main content

Tenzi za Rohoni 121 – Liko Lango Moja Wazi

Tenzi za Rohoni 121 – Liko Lango Moja Wazi

Tenzi Na. 121

Soma maneno kamili ya Tenzi za Rohoni namba 121, “Liko Lango Moja Wazi”, kwa ajili ya ibada, kuimba na kujifunza.


Maneno ya Wimbo

Liko lango moja wazi,
Ni lango la mbinguni;
Na wote waingiao
Watapata nafasi.
Lango ndiye Yesu Bwana
Wote waingie kwake,
Lango! Lango
La Mbinguni ni wazi.
Yesu ndiye lango hili,
Hata sasa ni wazi,
Kwa wakubwa na wadogo,
Tajiri na maskini.
Hili ni lango la raha,
Ni lango la rehema;
Kila mtu apitaye
Hana majonzi tena.
Tukipita lango hili
Tutatua mizigo,
Tuliochukua kwanza,
Tutavikwa uzima.
Hima ndugu tuingie
Lango halijafungwa,
Likifungwa mara moja
Halitafunguliwa.


Tazama Tenzi za Rohoni 1–164


Omba App ya Tenzi za Rohoni kwa Android

Scroll to Top